Na Shushu Joel, Pwani
MWENYEKITI wa Jukwaa la Ukuaji Kiuchumi kwa Wanawake Mkoa wa Pwani Bi, Mariam Ulega amekoshwa na uwingi wa wanawake katika Mkoa huo ambao wanajishughulisha na ujasiloamari mdogo mdogo.
![]() |
Bi, Mariam Ulega akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wajasliamali waliojitokeza kuonyesha bidhaa zao ( NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na wajasiliqmali hao waliojitokeza kuonyesha bidhaa zao katika siku ya sherehe za utoqji wa Tuzo mbalimbali zilizo andaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Mwanamke Sahihi Fete Mariam Ulega alisema kuwa hii ni hatua kubwa sana kwa Wanawake kuweza kuongeza juhudi za kupambana.
Aliongeza kuwa Wanawake wengi sasa wamekuwa wapambanaji sana katika kujiongezea kipata na kukuza uchumi wa Taifa letu na hii yote chanzo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuifungua nchi .
Hivyo Mariam Ulega amempongeza Rais Dkt Samia kwa ushupavu anaouonyesha kwa kuwa mwanamke pekee anayepambana kukuza uchumi wa Taifa kupitia vitu mbalimbali ikiwemo utalii na viti vingine ambavyo vimekuwa na tija kubwa kwa Taifa.letu.
Aidha Mariam Ulega amewaunga mkono wajasiliamari wote waliojitokeza kwenye hafla hiyo kwa kuwaunga mkono kwa kununua mahitaji ya wote waliojitokeza .
"Tuendelee kupambana na shughuli zetu tunazozifanya kwani ndizo nguzo za maendeleo yetu" Alisema Bi, Mariam Ulega
Kwa upande wake mmoja wa wajasiliamali Mwajuma Ally waliojitokeza kwenye hafla hiyo na wamechagiwa bidhaa zao na Mariam Ulega amempongeza kwa moyo wake wa kujitolea kwa jamii.
MWISHO
0 Comments