Na Shushu Joel, Katavi.
NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Dotto Mashaka Biteko amewataka jumuiya ya Wazazi nchini kuendeleza Upendo,Umoja na Mshikamano katika jumuiya hiyo kwa kusudi la kujenga jumuiya.
| Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Biteko akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza la wazazi Taifa (NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akifungua mafunzo kwa ajili ya kujengewa uwezo kwa baraza la Umoja wa Wazazi Taifa.
"Tukipendana , Tukithaminiana na kushikamana Chama hiki kitazidi kuwa Chama bora na chenye kuigwa nje ya mipaka ya Tanzania" Alisema Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko
Aidha amewataka wajumbe kuongeza umakini kwa elimu wanayoenda kuipata kwa kusudi la wao kwenda kusaidia jamii kule kwenye makazi yao.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndg, Fadhil Maganya amempongeza Naibu Waziri Mkuu kwa ushiriki wake wa ufunguzi wa semina ya wajumbe wa Baraza kuu la jumuiya ya Wazazi Taifa ambalo limefanyika Mkoani Katavi.
MWISHO
0 Comments