DKT BITEKO AELEZA MAFANIKIO YA RAIS DKT SAMIA NDANI YA BUKOMBE.

 Na Shushu Joel, Bukombe 


MBUNGE wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko amewataka wananchi wa kata ya Lyambamgongo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu wake mkubwa wa kuwahudumia watanzania.

Dkt Biteko akizungumza na wananchi wa kata ya Lyambamgongo wilaya ya Bukombe Mkoani Geita katika ziara yake ya kuzungumza na wananchi. (NA SHUSHU JOEL)


Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara katika kata hiyo Dkt Biteko  alisema kuwa kwa jinsi ambavyo Wilaya yetu ya Bukombe ilivyokuwa na ilivyo sasa kuna mabadiliko makubwa sana kwenye maendeleo ndani ya Wilaya yetu ya Bukombe.


"Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametuletea miradi  mingi katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Maji, Miundombinu, Umeme na mingine mingi katika Wilaya yetu ya Bukombe" Alisema Dkt Biteko 


Aidha alisema kuwa kwa jinsi ambavyo Rais Dkt Samia amefanya maendeleo kwetu Bukombe si hapa tu bali ni nchi nzima hivyo ndio muone jinsi gani Rais wetu amekuwa mwenye uchu wa maendeleo na Taifa hili.


Pia Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Biteko amewasisitiza wananchi wa Bukombe kuweza kujitokeza kujiandikisha kwenye daftali la kupiga na Kisha kumpa zawadi ya pekee Rais Dkt Samia ambayo ni kura nyingi za ccm katika uchaguzi wa serikali za mtaa.


Naye Diwani wa kata hiyo ya Lyambamgongo Ndg Boniface Shitobela akizungumza kwa niaba ya wananchi amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko kwa kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Bukombe katika ufanikishaji wa maendeleo.


Aidha amewataka wananchi kuwa walinzi wa miradi ya maendeleo kwani kuna watu wengine sio wema katika ulinzi wa miradi hiyo.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments