"MTUMIENI VYEMA WAZIRI ULEGA" HAPI


Na Shushu Joel, Mkuranga 


KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Taifa (CCM) Ndugu Ally Hapi amewataka wana CCM na wananchi wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kumtumia vyema Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ili ile tamaa yake ya kufanikisha ndoto yake ya maendeleo yanawafikia wana Mkuranga. 

Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Ndugu Hapi akitoa neno kwa wananchi wa Mkuranga ( NA SHUSHU JOEL) 


Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo katikq viwanja vya stand ya mabasi.


Aliongeza kuwa Mhe. Ulega ni moja wa Mawaziri watendaji wa kazi  wenye uwezo hivyo ni vyema mkampatia ushirikiano wa kutosha katika ufanisi wa kazi zake.


Aidha alisema kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa ni kiongozi wa kielelezo hapa nchini kwa kutoa pesa nyingi za miradi ya maendeleo kila kona ya nchi hii.

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameguza nyanja zote za maendeleo ikiwemo Afya, Elimu, Maji, Umeme, Miundombinu.

Naye Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Mkuranga Ndugu Juma Mahege amempongeza katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kwa utendaji wake wenye kuiboresha jumuiya.


Pia amemwakikishia kuwa katika wilaya ya Mkuranga hakuna mtaa utakao potea kutokana na kile wanachokitaka wananchi kutoka kwa viongozi wao kupatikana.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments