Na Shushu Joel, Bukombe
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamethibitisha kuwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao ni mwepesi sana kwa chama Cha Mapinduzi kwa kuwa Chama hicho kimefanya maendeleo makubwa kwa wananchi
![]() |
Katibu wa CCM wilaya ya Bukombe Ndg Leonard Mwakalukwa akisisitiza jambo |
Akizungumza na HABARI MPYA BLOG Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo Ndg Leonard Mwakalukwa alisema kuwa ccm inauhakika na ushindi kutokana na kile kinachotekelezwa kwa wananchi juu ya maendeleo.
Aliongeza kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko amekuwa mtekelezaji mkubwa wa maendeleo kwa Wananchi wa Bukombe.
Hivyo kutokana na kile ambacho Wananchi wanakihitaji kuweza kuwepo tunaamini kuwa hakuna chama cha upinzani kitakachopata kura .
Naye Eliza Kuyonza amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina uhakika na ushindi wa chaguzi zote kutokana na kile ambacho kinafanywa kwao.
Aliongeza kuwa kutokana na jinsi maendeleo yanavyofanyika kwa wananchi kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya Barabara.
MWISHO
0 Comments