DKT BITEKO CHANZO CHA UKUAJI WA UCHUMI BUKOMBE


Na Shushu Joel, Bukombe 


WANANCHI wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko kwa kulifungua jimbo hilo kiuchumi kwa ujenzi wa barabara zinzotoka ndani ya kata kuelekea makao makuu ya wilaya.

Akizungumza na HABARI MPYA BLOG Bi, Eliza Kuyonza ambaye ni mkazi wa kata ya  Katente alisema kuwa kufunguka kwa Miundombinu ya Barabara kumechangia kukua kwa uchumi wa Wananchi mmoja mmoja kutokana na uwepesi wa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali .


Aliongeza kuwa awali kulikuwa na Changamoto kubwa ya usafirishaji kutokana na ubovu wa Barabara ambazo zilikuwa zikichangia kutumia muda mwingi ukiwa kwenye barabara jambo ambalo lilikuwa likichangia kuzolota kwa biashara.


Aidha Bi, Eliza amemsifu Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa wilaya ya Bukombe. 


Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa kata ya Bulega Diwani wa kata hiyo  Ndugu Erick Kagoma   wamemshukuru Mhe Mbunge ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko kwa mchango wake mkubwa anaozidi kuufanya kwa wananchi wa kata ya Bulega katika maendeleo mbalimbali kwenye kata hiyo ikiwemo Barabara, Afya, Maji na Elimu jambo ambalo limeibadilisha kata yetu.


Aidha aliongeza kuwa kata ya Bulega itaendelea kumuunga mkono kwa asilimia 100% Mbunge wa Jimbo ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko kwa kazi kubwa anazozifanya kwenye maendeleo.


Hivyo amewataka wananchi kuendelea kutunza na kulinda miradi hiyo ili iendelee kutumika kwa vizazi vyetu.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments