"DKT BITEKO NI KIONGOZI MWENYE UCHU WA MAENDELEO" WANANCHI


Na Shushu Joel, Bukombe 


WANANCHI wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko kwa kuwa kiongozi mwenye uchu wa maendeleo kwa wananchi wake.

Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko akifafanua jambo katika moja ya vikao vyake


Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti wananchi hao kila mmoja anekuwa na muonekano tofauti huku kikubwa wakimsifia Mbunge wao Dkt Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha maendeleo yanakuwa kwa kasi katika wilaya ya Bukombe. 


Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata Busonzo Diwani wa kata hiyo Mhe Safari Mayala alisema kuwa kwa kipindi alichoongoza Mbunge wetu Dkt Biteko ni hatua kubwa ya maendeleo imefanyika kwa wananchi wa Bukombe .


Jimbo la Bukombe lilikuwa na giza kwani ni sehemu chache zilizokuwa na umeme lakini ndani ya uongozi wa Dkt Biteko kila kijiji kina umeme.


Aidha Mhe Safari aliongeza kuwa wilaya ya Bukombe inaendelea kukua kwa kasi katika nyanja zote za maendeleo jambo ambalo linasukumwa kwa kasi na Mbunge wetu Dkt Biteko. 


Kwa upande wake Diwani wa viti maalum Bi, Rahel Sololo mara baada ya kufanya mahojiano na HABARI MPYA BLOG alisema kuwa Mbunge wetu Dkt Biteko katupa heshima kubwa Wanawake wa Bukombe kwani upatikanaji wa maji safi na salama  umezidi kuwa mkubwa kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali wakati jambo hili awali ilikuwa ni changamoto kubwa.


Hivyo Diwani Sololo amempongeza Mbunge Dkt Biteko kwa kuwa kiongozi mwenye utatuzi wa changamoto za jamii hakika Dkt Biteko ni kiongozi mwenye uchu wa maendeleo na wananchi wa Bukombe 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments