WANANCHI NAMONGE WAELEZA JUZI YAO ILIVYOBADILISHWA NA DKT BITEKO


Na Shushu Joel, Namonge 


WANANCHI wa kata ya Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa kuwatoa kwenye giza nene na kuwaweke kwenye Nuru ya maendeleo.


Kata ya Namonge ni miongoni mwa kata zilizopo katika Jimbo la Bukombe na ndio kata kubwa kuliko zote na ni miongoni mwa kata zinazo ongoza kwa kilimo cha viazi vitamu kama biashara.


Akizungumza kwa machungu Diwani wa kata hiyo Ndugu  Mlalu Bundala alisema kuwa kata hiyo ilikuwa na changamoto kubwa ya barabara jambo ambalo lilipelekea kudolola kwa maendeleo kwenye kata hiyo kutokana na safari ya kutoka Namonge kwenda Runzewe ilivyokuwa ikiwaxhukua muda mrefu.


Aiidha alisema kuwa Wananchi wa Namonge walikuwa duni kutokana na mazao yao ya kibiashara kutokuwa na thamani hii yote ilitokana na changamoto ya barabara iliyokuwa ikisababisha .


Hivyo uwepo wa Dkt Biteko katika nafasi ya Ubunge umepelekea kuiinua kata hiyo kiuchumi mara baada ya kujengwa kwa barabara ambayo inapelekea magari kupita kwa uhakika na kuwafikia wakulima na kuuza biashara zao kwa bei nzuri ambazo zinapelekea wakulima kunufaika na kilimo huku uchumi wao ukizidi kukua kila kunapokucha hivyo Mbunge wetu Dkt Biteko ametutoa kwenye juzi ya giza na kutuweka kwenye Nuru ya sasa yenye Mwanga.


Naye Mashiku Masalu mmoja wa wakulima walionufaika na kilimo cha viazi anasema kuwa Dkt Biteko ni chanzo cha mafanikio yake kutokana na jinsi ambavyo ameitoa Namonge kwenye giza na kuiweka kwenye Nuru


MWISHO

Post a Comment

0 Comments