TIRA YAPONGEZWA KUTOA ELIMU YA BIMA MKOANI KATAVI


Na IRENE TEMU,Katavi


Mkuu wa  Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf,ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida za bima pindi majanga yanapotokea.


 Ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TIRA katika maonesho ya wiki ya Mwanakatavi yanayoendelea katika uwanja wa CCM Azimio Manispaa ya Mpanda.


Nakutoa rai kwa wakulima,wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kufika katika banda la Mamlaka ya usimamizi wa bima kupata elimu.


"kwani tunaishi lakini hatujui tutapata janga gani na kwa wakati gani,tuna wakulima wakubwa sana ambao wanaweka pesa nyingi katika Kilimo sawa na wanunuzi wa magari ya bei kubwa wanabima,hivyo wakulima waje katika banda hili wapate elimu nao wakate bima"DC Jamila


Aidha,ameongeza kuwa ukiwa na bima unakuwa na wakati mzuri wa kupata fidia na kukinga biashara pindi unapopata majanga.


Kwa upande wake Meneja wa TIRA Kanda ya Ziwa Tanganyika Kurenje Mbura,amewahamasisha wakazi wa Mkoa wa Katavi kuchangamkia fursa ya biashara ya bima kwani ni biashara yenye faida kubwa na katika Mkoa wa Katavi wanaofanya biashara ya bima ni wachache sana.


Kurenje amewataka pia wakulima na wadau mbalimbali  wa uzalishaji kukata bima ili kuweza kupata fidia pindi wanapopata changamoto ya mafuriko au uzalishaji wa mazao kuwa chini.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments