KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA WAKUFUNZI UVCCM BUKOMBE WAPIGWA MSASA


Na Shushu Joel, Bukombe 


KUELEKEA Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi huu mwishoni uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita umewapiga msasa wakufunzi wa jumuiya hiyo.

Mwenyekiti Uvccm wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao kazi (NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa kikao kizito cha maelekezo kwa wakufunzi hao Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndugu Nelvin Salabaga alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na kusudi la kuwakumbusha wajibu wao wa kila siku ndani ya uongozi wao.


Aidha alisema kuwa Umoja wa vijana umekuwa na mambo mengi hivyo ilikuwa ikiwapelekea baadhi ya wakufunzi kusahau wajibu wao wa kila siku ndio maana tumekutana ili kuweza kuwakumbusha wajibu wao ndani ya jumuiya na Chama kwa ujumla.


Pia Ndugu Salabaga alisema kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Chama Cha Mapinduzi kinakwenda kushinda viti vyote kwani serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya maendeleo makubwa katika Wilaya ya Bukombe huku Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko tumemuomba asije  kwenye uchaguzi huo kwani aliyofanya ni ushindi mkubwa unakuja ndani ya CCM.


Kwa upande mmoja wa wakufunzi hao Ndugu Kanu Selemani amempongeza Mwenyekiti huyo kwa kuwakumbusha wakufunzi hao majukumu yao ya kila siku na hasa kuelekea kipindi hiki cha Serikali za Mitaa. 


Aidha amewakumbusha wakufunzi wenzake kuzingatia yote yaliyokumbushwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments