"VIJANA TUCHANGAMKIE MIKOPO YA DKT SAMIA " MANJALE


Na Shushu Joel, Geita 


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Geita Ndugu Manjale Magambo amewataka vijana wa Mkoa huo kuhakikisha wanachangamkia fursa za mikopo ya halmashauri ambayo inatolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan. 

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Geita Ndugu Manjale akionyesha ishara ya mitano tena kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan(Na Shushu Joel) 


Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa huo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo kutoka kila Wilaya ndani ya Mkoa huo.


Manjale alisema kuwa ni vyema vijana kuhakikisha wanachangamkia mikopo hiyo ili kila mmoja kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha biashara mbalimbali ambazo zitakwenda kuwa suluhu za mahitaji yao.


Rais Dkt Samia ni kiongozi ambaye amekuwa na uchu wa mafanikio ya vijana hivyo ameamua kurejesha mikopo hiyo ambayo hapo awali ilisimamishwa kwa makosa mbalimbali. 


Aidha Mwenyekiti Manjale amewakumbusha Wakurugenzi wa halanshauri kuweza kuwapa kipaumbele vijana ambao ndio walengwa wakubwa wa mikopo hiyo.


Pia amewataka vijana kuwa waungwana katika kurejesha mikopo hiyo ili iweze kuendelea kuwapatia na watu wengine ili nao waweze kupata kunufaika na mikopo hiyo.


Naye Amina Abdallah amempongeza Mwenyekiti huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika masuala ya vijana na hasa katika kukuza uchumi wao.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments