WAZIRI MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA KILELE CHA KONGAMANO LA TEHAMA

Na Mwandishi wetu 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 17, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.


Akizungumza baada ya kutembelea mabanda  ya Maonesho kwenye Kongamano hilo, Mheshimiwa Majaliwa  ameipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanasimamia ukuaji wa Sekta ya TEHAMA.


Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amewataka vijana kutumia fursa ya Uwekezaji unaofanya na Serikali katika sekta ya TEHAMA ili kukuza uchimi binafsi na Taifa kwa ujumla


Kaulimbinu ya Kongamano hilo ni “Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Robotiki kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii".

Post a Comment

0 Comments