Na Shushu Joel, Bukombe.
MBUNGE wa Jimbo la Bukombe , Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko amezidi kuwa Mwalimu wa siasa safi yenye mashiko makubwa kwa jamii ambayo malengo yake ni kuwatoa watu gizani na kuwa kwenye Nuru.
Hivi karibuni Dkt Biteko amesikika akisema watu wote hapa ni wale wale na wakati wote unawahitaji watu uwe na fedha usiwe na fedha unawahitaji watu na hata ukifa utazikwa na wa watu msemo ambao umekuwa na hisia kubwa kwa watanzania .
Dkt Biteko amekuwa kiongozi wa aina yake kwa kutoa hotuba zake zenye kuvutia na zinzotoa funzo kubwa kwa watanzania ambazo pia zinawanufaisha watanzania kutoka gizani na kwenda katika Nuru.
Hivyo kama watanzania wameshauliwa kutumia hotuba za Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko kuwa kama ni funzo ili ziweze kuwa msaada mkubwa kwa kuweza kujifunza mambo mbalimbali.
Abel Mkingwa ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakifuatilia hotuba za Dkt Biteko alisema kuwa Dkt Biteko ni kiongozi wa kuigwa kwa jamii kutokana na kile anachokifanya kwa watanzania.
Aidha amewataka watanzania kuendelea kufuatilia hotuba za Dkt Biteko kwani zimekuwa na elimu kubwa zenye kujenga kwa jamii.
MWISHO
0 Comments