Na Shushu Joel, Mafia.
KATIBU tawala Wilaya ya Mafia Ndugu Shabani Shabani amewataka vijana Nchini kuendelea kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliachwa na Waasisi wa Taifa letu.
Akizungumza na HABARI MPYA MEDIA Ndugu Shabani alisema kuwa Waasisi wetu Hayati Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume waliona mbali sana na kisa kufanikisha Muungano huo.
Aidha amewataka vijana kuendelea kuyaenzi mawazo ya waasisi hao ambao waliamua kutengeneza umoja huo ambao umezidi kuwa chachu kwa mataifa mbalimbali kutokana na jinsi ambavyo umezidi kudumu kwani mpaka sasa Muungano huo unatimiza miaka 61.
Juma Ally ni mmoja wa vijana wakazi wa Wilaya ya Mafia amesema kuwa Muungano ni Tunu kubwa tuliyoaachiwa na waasisi hivyo kila kijana anatakiwa kuwa mlinzi wa Muungano huo.
MWISHO
0 Comments