MIRADI YA ZAIDI YA BILIONI MOJA YATEMBELEWA NA MWENGE KISARAWE


Na Shushu Joel, Kisarawe 


MWENGE wa Uhuru umezindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni moja katika Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani .



Miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo ni Taa za barabarani,Mradi wa Maji,Bweni na shule ambayo yote kwa ujumla inakamilisha kiasi hicho cha pesa.


Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia Mwenge huo kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi ameupongeza uongozi wa wilaya ya kisarawe chini ya Mkuu wa Wilaya Petro Magoti .


Aidha amewataka kuendelea kuitunza miradi hiyo iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Pia Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge amesisitiza kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana kwani Taifa linawategemea katika mambo mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments