"BUNGE KUMPA TUZO RAIS SAMIA NI ISHARA YA USHINDI WA CCM KILA JIMBO" MNEC NADRA GHULAM


Na Shushu Joel, Dodoma


BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiongozwa na spika wake Dkt Tulia Akson limemkabidhi Tuzo maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuonyesha upendo wa hali ya juu na uchapa kazi wake.



Kupatiwa kwa Tuzo hiyo maalum Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Dkt Samia kinakwenda kupata ushindi wa kishindo katika kata na Majimbo kupitia wagombea wake watakao pewa nafasi za kupeperusha bendera za chama.


Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Nadra Ghulam. 


Alisema kuwa watanzania tuna kila sababu ya kujifunia mafano ya kipindi cha miaka minne yaliyofanywa na Rais wetu .


Pia Mnec Nadra Ghulam alisema kuwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt Samia hakuna kilichosimama hii ikiwa na maana miradi yote imetekelezeka kwa kiwango cha hali ya juu.


Hivyo niwaombe watanzania kuendelea kumwamini kiongozi wetu na tumpe nafasi hiyo kwa kipindi hiki kinachokuja ili amalizie kazi mdogo mdogo kwa  watanzania ambazo zimebaki.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments