Na Shushu Joel , Bukombe
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Nelvin Salabaga ameeleza kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko amekuwa chanzo cha kupukutika kwa upinzani katika jimbo hilo.
Akizungumza na HABARI MPYA BLOG Mwenyekiti huyo alisema kuwa kipindi cha nyuma uongozi wa jimbo letu ulikjwa upinzani hivyo Bukombe ilikuwa nyuma sana katika maendeleo.
Aidha aliongeza kuwa tangu Dkt Biteko ashikilie jimbo kumekuwa na mabadiliko makubwa ya maendeleo katika jimbo la Bukombe jambo ambalo limepelekea kupukutika kwa upinzani Bukombe.
"Kwa kweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Dkt Biteko amekuwa Mbunge wa pekee katika Jimbo letu pia hii ni kama tunu ambayo wanabukombe tumetunukiwa na Mungu" Alisema Mwenyekiti Ndgu Salabaga.
Naye Masanja Juma amempongeza Mwenyekiti wa Wilaya kwa maono yake ambayo amekuwa akiyafanya kwetu vijana.
MWISHO
0 Comments