Na Shushu Joel, Dodoma.
MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi, Nadra Ghulam amesema kuwa Ilani ya CCM ya 2025- 2030 ni mwendo wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya kusomwa kwa ilani hiyo MNEC Ghulam alisema wananchi wakae mkao wa kula maendeleo kwa kipindi hiki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kuiona Tanzania inapiga hatua kubwa zaidi ya miaka 4 anayomalizia.
Aidha amesema kuwa atatembea sehemu mbalimbali kuhakikisha anaielezea ilani hiyo iliyojaa maendeleo kwa wananchi na imani yangu mengi yanaenda kutekelezeka bila wasiwasi.
MWISHO
0 Comments