"HAKUNA WA KUZUIA UCHAGUZI OCTOBER 2025" MNEC GHULAM


Na Shushu Joel, Bagamoyo

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Nadra Ghulam amewataka watanzania kutokuwa na hofu yeyote ile juu ya wapotoshaji kuhusu uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October mwaka.


Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Mnec Ghulam alisema kuwa kuna kikundi cha watu cha ovyo ambacho kimekuwa kinstangaza kutokuwepo kwa uchaguzi Mkuu jambo ambalo ni la uongo na watu hao wanatakiwa kupuuzwa.


"Uchaguzi wetu upo pale pale kama ilivyopangwa na Tume ya uchanguzi hivyo sasa Watanzania msiogopeshwe na makelele ya chula" Alisema Mnec Nadra Ghulam 


Aidha amewataka wananchi kupuuza kelele zao za matusi kwani ni sawa na maneno ya wahenga ambapo walisema kuwa mfa maji aachi kutapatapa.


Pia Mnec Ghulam amekoshwa na miradi ya elimu katika wilaya ya Bagamoyo ambayo inafanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Kwa upande wake Mkazi wa Bagamoyo Ibra huruka amemhakikisha Mnec Nadra Ghulam kuwa hakuna kitakachobadilika kuendelea uchaguzi Mkuu kwani wana Bagamoyo tunakwenda na Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Aiha amewataka wananchi kutokuyumbishwa na matusi ya mitandaoni kwani hao ni wachumia matumbo.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments