MHE MGALU AELEZA MAONO YA ILANI YA CCM 2025- 2030
Na Shushu Joel, Mkuranga
MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Mhe Subira Mgalu amewataka wananchi wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani na watanzania kwa ujumla kuendelea kukaa Mkao wa kula kwani yaliyoma kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mapinduzi makubwa katika maendeleo.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwalusembe Mhe Mgalu alisema kuwa ilani ya ccm inakwenda kuwainua vijana kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujuzi kupitia veta na kisha kuwapa mitaji ili kuyafanya kwa vitendo yale walioyapata kule veta.
Aidha alisema kuwa katika miundombinu ya barabara ilani yetu inasema inakwenda kutengeneza barabara za kiwango cha lami na kuzifanya zile za tarura kupitika vipindi vyote bila wasiwasi ,Pia Ilani ya ccm inakwenda kusambaza umeme kwenye vitongoji vyote vilivyobaki.
"Hakika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kapania kuwashushia maendeleo watanzania hivyo tuendelee kukaa mkao wa kula" Alisema Mbunge wa Mkoa wa Pwani Mhe Subira Mgalu.
Hivyo amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi ili kizidi kuwaletea maendeleo
Kwa upande wake Juma Shabani Mkazi wa Mwalusembe amempongeza Mhe Mgalu kwa kuwasomea ilani ya mwaka 2025-2030 kwani inamatumaini makubwa kwetu wananchi hasa tuliposikia upanuzi wa barabara ya Lindi jambo ambalo linakwenda kukuza uchumi wetu.
MWISHO
0 Comments