MHE MGALU ASHUSHA NEEMA UWT BAGAMOYO


Na Shushu Joel, Bagamoyo 


MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Mhe Subira Mgalu ameshusha neema kwa viongozi na wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia jumuiya ya umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mara baada ya kutatua changamoto ya usafiri kwa kuwapatia gari aina ya Noah.


Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo Mhe Mgalu alisema kuwa moja ya nadhili aliyojiwekea kipindi cha nyuma ilikuwa ni kuhakikisha anainunulia chombo cha usafiri jumuiya hiyo kwa kusudi la kurahisisha utendaji kazi wa jumuiya hiyo.


Aidha aliongeza kuwa ni vyema gari hilo likatumike kutafuta kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu huko kwenye matawi kwa kuwakumbusha wananchi kile kilichofanyika kwenye maeneo yao.


"Gari hili likatumiwe na jumuiya zote za Chama ikiwemo Wazazi na Vijana ili ziweze kufanikisha malengo ya Chama chetu" Alisema Mbunge huyo wa Mkoa wa Pwani ( Mhe Mgalu) 


Akikabidhi Gari hilo kwa Katibu wa  Wilaya ya Bagamoyo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi Mery Chatanda amempongeza Mhe Mgalu kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitoa kwa jumuiya hiyo.


Aidha amewataka viongozi wa Bagamoyo kuhakikisha wanaitumia gari hiyo kwa makusudio yaliyokusudiwa ili kurahisisha shughuli za utendaji wa jumuiya.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments