MGALU NI LULU YA BAGAMOYO


Na Shushu Joel, Bagamoyo 

WANA Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamempongeza Mbunge wa Mkoa huo Bi, Subira Mgalu kwa kusema kuwa kiongozi huyo ni sawa na Lulu iliyotelemshwa na Mungu.


Wakizungumza na HABARI MPYA BLOG Wananchi hao walisema kuwa kwa jinsi ambavyo Mbunge Mgalu amekuwa akijitoa kwenye masuala mbalimbali ya kijamii pasipo kujali dini wala Kabila inaonyesha kabisa Bi,Mgalu ni kiongozi mwenye maadili mema na yenye hofu ya kesho yake.



Naye Mwanahawa Hamja ambaye ni Mjumbe kamati ya utekerezaji uwt wilaya ya  bagamoyo amempongeza Mhe Mgalu kwa kuosaidia jumuiya kwa kiwango cha hali ya juu katika masula mbalimbali ila kubwa ni la kutoa gari kwa lengo la kusaidia viongozi ili waweze kuwafikia wanachama wa ngazi za chini.


Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama hicho Wilaya ya Bagamoyo Ramadhani Lukanga alisema kuwa Mhe Mgalu amekuwa nguzo imara sana katika kuhakikisha ccm inapata ushindi wa kishindo ndio maana ametoa gari kwa ajili ya kwenda site na kuwafikia wanachama kwa wepesi.


Aidha amemtaka kuendelea kuwa na moyo huo wa kikisaidia Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kupata ushindi mnono kwa kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,Mbunge na Madiwani .

MWISHO 

Post a Comment

0 Comments