MNEC GHULAM AWANYOOSHEA KIDOLE VIONGOZI WASIOFANYA VIKAO

Na Shushu Joel, Mlandizi

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Nadra Ghulam amewaonya viongozi wote kuanzia ngazi za matawi mpaka Wilaya ambao wamekuwa na tabia ya kutokufanya mikutano na Wananchi wa maeneo yao.

Onyo hilo amelitoa alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wa kata ya Kibaha Vijijini ambapo amewataka kufanya vikao na wananchi kwa lengo la kutatua kero zao ambazo wengi wao wamekuwa wakiuliza mara baada ya viongozi wa kitaifa kufika kwenye maeneo yao jambo ambalo si sahihi.


Aliongeza kuwa viongozi wa chini wamekuwa wakikipa changamoto sana chama cha Mapinduzi kwa sababu wengi wao wamekuwa wavivu wa kufanya vikao dhidi ya wananchi wa maeneo yao hivyo niwatake kila mmoja aliyepewa dhamana ya kuwa kiongozi ni vyema wakafanya vikao.


" Wananchi wengi wamekuwa wakiwasilisha changamoto zao kwa viongozi wa kitaifa kutokana na kutokufanyika kwa vikao vya kujadili na kutatua changamoto zao" Alisema Mnec Nadra Ghulam 


Aidha alisema kuwa atahakikisha vikao vinafanyika kwa wananchi ili waweze kunufaika na Chama chao wanachokiamini katika kuwaletea maendeleo

"Endeleeni kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani ni chama pekee chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo " Alisema Mnec Ghulam 

Kwa upande wake Rajabu Issa Mkazi wa kata hiyo amemshukuru Mnec Ghulam kwa kuwakumbusha viongozi hao majukumu yao ambayo wengi wao wameshindwa kutekeleza na hasa kuwepo kwa vikoa mbalimbali vya kujadili maendeleo.


Aidha alisema kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni kuwa hapa kibaha kijijini hakuna kura ya Rais Dkt Samia itakayopotea na hii ni kutokana na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments