WAZIRI KIKWETE ATOA NENO PPRA

 Nimeshiriki na kuhutubia Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya PPRA lililolenga kujadili Ununuzi wa umma na Ukuzaji wa kampuni za wazawa na makundi maalum kwa ukuaji wa Uchumi Jumuishi katika zama hizi za mabadiliko ya teknolojia/ Kidigitali lililofanyika Jijini Arusha

Katika hotuba yangu, nimewakumbusha umuhimu wa kuendelea kutambua kuwa mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan , Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanalengwa pamoja na mengineyo kuwasaidia na kukuza ustawi wa Watu wenye mahitaji maalum. Pia nilitumia nafasi hiyo kubainisha kwa

Kuwakumbusha mambo 6  yaliyofanywa na  Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwawezesha vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kujiinua kiuchumi ikiwemo maelekezo ya kisheria ya kuendelea kutenga Asilimia 30 ya zabuni za ununuzi wa umma. 


Pia nilitumia nafasi hiyo

Kuwakumbusha umuhimu wa kutoa elimu na kuwashirikisha wadau muhimu katika jamii wakiwemo Madiwani na Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji ili elimu ya kuwepo kwa fedha maalum zinazotengwa toka kwenye manunuzi ya Umma ijulikane kwani moja ya changamoto kubwa kwa sasa ni ufahamu hafifu wa kuwepo kwa fedha hizi. Umuhimu na msisitizo kama huu umesaidia sana vijana, wanawake na wenye ulemavu kukimbilia zile asilimia 10 zinazotengwa na Halmashauri kutoka kwenye mapato ya ndani. 


Nilimaliza kwa kuwashukuru sana PPRA kwa kazi nzuri na kutambua umuhimu wa kuandaa kongamano hili ambalo kwa hakika linalenga kuwawezesha wananchi. Kwani kufikia kwa malengo haya ni kuwawezesha Watanzania.

Post a Comment

0 Comments