"LENGO LA RAIS SAMIA NI KUSOGEZA HUDUMA ZA JAMII KARIBU " MNEC GHULAM


Na Shushu Joel, Mkuranga 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye maono makubwa dhidi ya watanzania kwa kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wote.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Mwalusembe Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani  Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania  Bi Nadra Ghulam alisema kuwa Rais Dkt Samia anamakudi ya kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ndio maana amezidi kuporomosha miradi ya maendeleo kwa jamii.


" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anahitaji huduma za uhakika kwa wananchi ziweze kuwafikia mahali walipo" Alisema Mnec Nadra Ghulam 


Pia Mnec Ghulam amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani ndio Chama pekee chenye dhamira kubwa ya kuwapatia maendeleo. 


Aidha amewataka wananchi wa Mkuranga kuifuatilia ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwani imebeba maono na matumaini makubwa kwa wananchi.


Kwa Upande wake wake Ally Juma (47) Mkazi wa kata hiyo ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani maendeleo ambayo tulikuwa tukiyaota na sasa yanetufikia hadi vijijini jambo ambalo ni nzuri na la kuigwa kwa viongozi wanaopata nafasi ya kutuongoza.


Aidha amewataka wananchi kuendelea kutunza miradi inayotolewa na serikali ili iendelee kutumika kwa vizazi vijavyo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments