"TAKUKURU YAWATAKA VIJANA WA SKAUT KUACHA UOGA KUTOA TAARIFA ZA RUSHWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI

Na Shushu Joel. Bukombe


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imewataka vijana kuacha uoga wa kutoa taarifa pindi wanapoona kuna viashiria vya Rushwa vinataka kufanyika.

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Takukuru wa  Wilaya hiyo Ndugu Said Mhina alipokuwa akizungumza na vijana wa *Skauti* wa Wilaya hiyo.


Alisema kuwa vijana lazima muwe Wazalendo kwa Taifa lenu ili kuweza kutokomeza vuashirilia vya Rushwa ambavyo vinaweza kujitokeza katika jamii zetu hivyo kila mmoja wetu atumie elimu hii kuwa  Mzalendo wa kweli katika kupambana na masuala ya Rushwa. 


" Rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya Taifa letu hivyo kila kijana anatakiwa kuwa mstari wa mbele katika masuala ya kuoambana na Rushwa " Alisema mkuu wa TAKUKURU ndugu Said Mhina.


Aidha amewataka vijana hao kwenda kuwa vipaza sauti kwa jamii zao kwa kuendeleza kutoa elimu waliyoipata ili sumu ya kupokea au kutoa Rushwa ikazidi kukemewa kwa kizazi hadi kizazi.


Kwa Upande wake Thomas Thomas Mkufunzi wa Sca ut Wilaya hiyo ameipongeza TAKUKURU kwa jinsi ambavyo imekuwa mstali wa mbele katika utoaji wa elimu kwa vijana juu ya masuala ya kuepukana na Rushwa.


Aidha aliongeza kuwa elimu tuliyoipata kutoka kwa Taasisi ya kupambana na masuala ya Rushwa inakwenda kusambaa kwa kasi wilaya ya Bukombe kutokana na jinsi ambavyo vijana wengi wamekuwa na uelewa wa hali ya juu.


Pia amewataka vijana wenzake kutumia elimu hiyo kuisambaza kwa jamii ili nayo ipate uelewa wa hali ya juu kuhusiana na masuala mazima ya Rushwa.

Post a Comment

0 Comments