BAGAMOYO KAENI MGUU SAWA KWA MAENDELEO" MHE MGALU

Na Shushu Joel, Bagamoyo 

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo  Mkoani Pwani Mhe Subira Mgalu amewataka Wananchi wa Jimbo hilo kukaa mguu sawa kwani yajayo ndani ya jimbo la Bagamoyo yanafurahisha .


Akizungumza kwa njia ya Simu kutokea Mkoani Dodoma Mbunge huyo alisema kuwa kiu yake ni kuona maendeleo yanawafikia wananchi wa Bagamoyo kupitia serikali yao ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 


"Naamini kwa jinsi ambavyo serikali yetu imajipanga kila kona kutakuwa na maendeleo" Alisema Mhe Mgalu 


Aidha amewataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali ya awamu ya sita ili izidi kutekeleza ahadi zake kwa vitendo. 


Bushiri Kitomboi ni mkazi wa Bagamoyo anasema kuwa wanabagamoyo wana imani kubwa na Mbunge wao kwani tangu akiwa viti maalum aliyoyafanya Mkoani Pwani yameonekana .

MWISHO

Post a Comment

0 Comments