Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (Uvccm) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu. Nelvin Salabaga anaungana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป katika kusimama kidete katika kudumisha na kulinda Amani ya nchi yetu na kuwataka Wana Bukombe i na Taifa kwa ujumla kusherehekea siku ya uhuru kwa utulivu tukiwa nyumbani kwetu.
Aidha amewataka vijana kutambua kuwa wao ndio viongozi wa Taifa hili hivyo wasikubali kudanganyika na visenti ambavyo ni hatari kwa hatma ya Nchi yao kesho.
"Tanzania ndio nchi yangu sina pahala pengine pa kwenda sitaki kuwa mtumwa" Ndg Salabaga
MWISHO

0 Comments