TAASISI ya Bilal Muslimu Mission Julai 12 imemkabidhi baskeli ya miguu mitatu Salum Lila mkazi wa Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambaye ana ulemavu wa miguu.
![]() |
| Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission Anwar Melali akimkabidhi Salum Lila baiskeli ya mataili matatu. Picha na Omary Mngindo |
Katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mbali ya viongozi wa taasisi hiyo, Mkuu wa wilaya Zainab Kawawa aliyewakilishwa na Katibu Tawala Kasilda Mgeni, akiwemo Kawambwa ambapo pia walikabidhi matenki madogo 9 na sabuni kwa ajili ya shule tatu ikiwa ni kudhibiti ugonjwa wa Corona.
![]() |
| Anwar Melali akimkabidhi Kasilda Mgeni matenki 9 ya maji yatayokabidhiwa kwenye shule tatu wilayani hapa, anayeshuhudi ni Mbunge aliyemaliza muda wake Dkt. Shukuru Kawambwa. Picha na Omary Mngindo. |
"Pia kuna mahusiano mazuri kati Kawambwa na Kawawa kwani wamekuwa na ukaribu wa kazi mbalimbali, lakini kwaniaba ya Mkuu wa wilaya na wana-Bagamoyo shukrani zaidi nizilete kwenu kwa ukarimu mkubwa kwa wananchi wetu," alisema Kasilda.
![]() |
| Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission Anwar Melali akimkabidhi Salum Lila baiskeli ya mataili matatu. Picha na Omary Mngindo. |
Akitoa shukrani kwa wana-Bilal Muslim, Kawambwa alisema kuwa taasisi hiyo imejitoa kwa kiasi kikubwa katika kuwatumikia wana-Bagamoyo katika sekta mbalimbali, ikiwemo tiba ya macho waliyoitoa miezi michache iliyopita ambapo wakazi zaidi ya 3,000 walipatiwa huduma hiyo pasipomalipo.
"Kwaniaba ya wana-Bagamoyo tunawashukuru sana viongozi wa Bilal kwa namna wanavyojitoa katika kutuaaidia katika nyanja mbalimbali, kwa niaba ya wananchi tunaendelea kuwaombea dua muwe na afya njema muendelee kututafutia wafadhili zaidi wake kutusaidia zaidi," alimalizia Kawambwa.
Kwa upande wake Lila akitoa neno la shukrani kwa Kawambwa, alianza kumshukuru kwa jitihada zake, huku alisema anamuombea dua arejee kwenye nafasi hiyo ili aendelee kiwasaidia wengine wenye mahitaji mbalimbali.
MWISHO




0 Comments