Na Shushu Joel.
RAIS wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Revocatus Kuuli.
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa
Kuuli leo Dec 28,2020 kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwaa ardhi ya
wananchi bila kufuata utaratibu,utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya
ya fedha za maduhuli ya Serikali.
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Aidha Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Phillemon Sangati
kuteua Kaimu Mkutugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja ili huduma za wananchi
ziendelee kufanyika kwa jamii
MWISHO
0 Comments