NA VICTOR
MASANGU, PWANI
SERIKALI mkoani Pwani imesema kwamba Kituo cha kupoozea umeme kilichopo mlandizi Wilayani Kibaha ambacho kilipatwa na majanga ya kuungua na moto mwezi machi mwaka jana hatimaye kimefanyiwa matengenezo na kinatarajia kuanza kufanya kazi rasmi mwezi machi 2021 ambapo kitatoa huduma ya utoaji wa nishati hiyo katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilayani za Kibaha pamoja na Bagamoyo.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist
Ndikilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kutembelea na
kujionea maendeleo na matengenezo mbali mbali katika kituo hicho ambapo
ameupongozeza uongozi wa Shirika la
umeme Tanesco Mkoa wa Pwani kuweza
kuboresha miundombinu ambayo ilikuwa imeharibika hapo awali na kuwa kero kubwa kwa wananchi hao kukosa umeme.
Ndikilo
alifafanua kwamba baada ya kutokea kwa janga la moto katika kituo hicho cha
umeme mlandizi baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali walikuwa
wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nishati hiyo ya umeme kutokana na
kukatika mara kwa mara lakini kutokana na juhudi ambazo zimefanyika na Tanesco
Mkoa wa Pwani kero hiyo sasa inakwenda kumalizika pindi ifikapo mwezi wa tatu
mwaka huu.
“Kwa kweli mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani nimefarijika sana na napenda kuchukua fursa hii kulipongeza sana ten asana Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani kutokana na kuonyesha nia ya kufanya yale yote ambayo tulikubaliana na kwa kweli kwa upande wangu nipende kusema kwamba nimeridhishwa na ukarabati na ujenzi ambao umefanyika hii ni dalili nzuri katika Mkoa wetu wa Pwani kuwa na nishati ya Uhakika.
Aidha Mkuu
huyo wa Mkoa wa Pwani alisema kwamba kwa sasa
mahitaji ya umeme Katika Mkoa ni
yanayohitajika ni mega watt zipatazo 117.8 na kwamba kukamilika na kuanza kutoa hudua kwa kituo
hicho ni moja ya kuleta maendeleo makubwa katika kukuza uchumi pamoja na
kuwavutia wawekezaji mbali wa ndani na nje ya nchi.
Kadhalika
alizitaka mamlaka nyingine ikiwemo
Dawasa pamoja na Tanrods kuhakikisha kwamba wanaweka mipango endelevu ya
kudhumisha huduma zao kwa wananchi ikiwemo kurekebisha miundombinu m bali mbali
ya barabra ili iweze kupitika kwa urahisi kuingia kwenye viwanda amabvyo vipo
katika Mkoa wa Pwani.
“Tanesco leo
kwa kweli nimetembelea kituo hiki cha kupozea umeme wamenirufarisha sana kwa
kuwa nimejionea mimi mwenyewe kwa jinsi walivyofunga mitambo na laini mbali mb
ali ambazo zinatumika katika kuwasambazia umeme wateja mbali mbali wa Wilaya ya
Kibaha pamoja na Bagamoyo pamoja na katika maeneo ya viwanda na hi ni hatua
kubwa kwa hivyo na taasisi zingine kama Dawawa na Tanrods na wao waige mfano
huu wasifanya kazi mezani ila wafanye kwa vitendo kama Tanesco.
Ndikilo pamoja na kulipongeza Shirika hilo la Tanesco Mkoa wa Pwani lakini pia amelitaka lifanye jitihada za makusudi katika kpelekeka umeme wa uhakika katika Wilaya ya Mkuranga ambayo nao inauwekezaji mkubwa wa viwanda na kujenga kituo maalumu cha kupozea umemem amabcho kitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuliko kutegemea kwa kiasi kikubwa umeme kutoka katika kituo cha Mbagala kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande
wake Meneja wa Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Mhandisi Mahawa Mkaka
amebainisha kwamba kituo hicho mwaka jana kiliweza kuungua na kusababisha
hasara kubwa na kusababisha changamoto kubwa ya baadhi ya maeneo kukatika katika kwa umeme mara kwa mara na
kwamba kituo hicho kitakuwa mkombozi
mkubwa kwa wananchi kupata umeme wa uhakika.
Naye Mkuu wa
kituo hicho cha kupozea umeme cha mlandizi Baraka Zonga kituo hicho cha
kupoozea umeme kina transfoma kubwa nne amabzo zitakuwa na uwezo wa kusambaza
umeme katika laini saba katika maeneo mbali mbali ikiwemo katika mitambo
ya maji ya ruvu juu pamoja na ile ya
ruvu chini sambamba na maeneo mengine ya viwanda na bandari kavu ya Kwala.
Mkoa wa
Pwani kwa sasa imetajwa kuwa kinara katika uwekezaji wa viwanda hivyo kuboresha
kwa miundombinu ya umeme na kuanza
kufanya kazi tena kwa kituo hicho
cha kupoozea umeme mlandizi kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi pamoja
na wawekezaji wa viwanda kupata umeme wa
uhakika.
MWISHO
0 Comments