Na Shushu Joel , Kisarawe
BARAZA la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani limeazima kwa pamoja kupitisha bajeti ya kiasi cha shillingi bilioni 39.8 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wake wa matumizi katika sekta mbali mbali ikiwemo miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2021 na 2022.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Joketi Mwegelo akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani ambacho kiliandaliwa kwa ajili ya kupitisha bajeti(NA SHUSHU JOEL)
Akitoa
taarifa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama wakati wa kikao cha baraza hilo
kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti hiyo kilichohidhuliwa na viongozi mbali mbali
wa serikali, taasisi za umma, wakuu wa idara
pamoja na wakuu wa vitengo kutoka mashirika ya umma ambao walialikwa
lengo la kutoa elimu kwa madiwani hao.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate
Mwegele amewaasa madiwani kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii na weledi ikiwemo kusikiliza changamoto
zinazowakabili wananchi na kuitifatua ufumbuzi lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali.
Pia Jokate
alisema kwamba serikali ya Wilaya ya Kisarawe itaendelea kutoa ushirikiano wa
kutosha kwa madiwani wote na watendaji
bila ubaguzi wowote kwa lengo la kuweza
kuwaletea wananchi maendeleo katika nyaja
bali mbali za maji, umeme
afya, na mambo mengine ya msingi kwa
kuzingiatia miongozo,taratibu na sheria
zote zilizowekwa za nchi.
Naye Mwenyekti wa Chama vcha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe Halfan Sika amelipongeza baraza hilo la madiwani kwa kuweza kushikamana kwa pamoja na kupitisha bajeti hiyo ambayo inakwenda kutatua au kupunguza kero na shida mbali mbali za wananchi wa maeneo mbali mbali ya Kisarawe.
Sika
aliongeza kuwa lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba
inaleta maenedeleo kwa wananchi wake kwa
kuzingatia utakelezaji wa ilani ya cahama katika yale mambo mbali mbali amabyo yameahidiwa ili
yaweze kufanyiwa kazi na kuleta mabadiliko katika Nyanja mbali mbali.
“Mimi
niwapongeza madiwani wote ambao kwa kweli mmeweza kufanya kazi kwa bidii katika
kuiandaa bajeti hii na kitu kikubwa ambacho tunapaswa kukifanya ni kuhakikisha
tunaweka mipango yetu vizuri ya kuweza kuwatumiakia wananchi wetu ikiwemo
kuwatatulia changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili na kuzitafutia
majawabu kwa hivyo nina imani kupita kwa
bajeti hii ni moja kati ya hatua katika maendeleo kwa wannachi wa
Kisarawe.”aliafafanua Sika.
Nao baadhi
ya madiwani wa baraza hilo akiwemo
Adamu Nimba na Mhandisi
Mohamed Kilumbi wameoumba uongozi wa
halmashauri hiyo ya Ksarawe licha ya kupisha bajeti hiyo lakini waongeze
ubunifu zaidi katikja suala zima la ukusanyaji wa mapato kwa kuwa ni vyanzo
vingine vipya ambayo vitaweza kuisaidia kuinua kiwango cha mapato.
“Sisi kama
baraza la madiwani hii bajeti
tumeipitisha lakini kitu kikubwa ni lazima kujipanga zaidi na kuwatumia
wataalamu wetu wa Kisarawe ambao wataweza kuzidisha kazi zaidia katika suala
zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kupitia njia mbali mbali za kubuni
vyavyo vipya vya muda mrefu katika
ukusanyaji wa mapato hayo,”alisisitiza Adamu.
Kadhlika
diwani huyo katika hatua nyingine alifafanua kwamba vyanzo vya mkaa na kuni ambavyo navyo
vinatumika katika ukusanyaji mzima wa kuingiza kipato lakini vitafikia wakati
vitakwisha hivyo kunapaswa kuwekwa mpango endelevu ambao utasaidia katika siku
za usoni kupata suala la upatikaniji wa
kuingiza mapato.
Halmashauri
ya Wilaya ya Kisarawe ni miongozi mwa halmashauri tisa zilizopo katika Mkoa wa
Pwani na ilianzishwa mnamo mwezi
Agosti mwaka 1962,ambapo kwa mwaka huu upitishwaji wa bajeti hiyo
itaweza kwenda kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kupunguza
changamoto za ukosefu wa huduma mbali
mbali ambazo zimekuwa zikiwakabiliwa wananchi
katika maeneo yao.
MWISHO

0 Comments