NA VICTA MASANGU
SERIKALI Mkoani Pwani kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa zao la Korosho wameazimia kwa pamoja kujenga ujenzi wa kiwanda kikubwa kwa ajili ya kuchakata zao la Muhugo ambacho kitajengwa katika eneo la Chailinze lililopo katika halmashaurli ya Chalinze Wilayani Bagamoyo kwa lengo la kuwakomboa wakulima wa zao hilo kuondokana na chanagamoto zinazowakabili katika soko.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere wa kulia akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Zamani ya Mkuranga wakiwa wanafuatilia mada mbali mbali ambazo zilikuwa zinatolewa katika kikao hicho cha wadau wa zao la korosho.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo ambaye alikuwa ni mwenyekiti katika mkutano huo alisema kwamba lengo kubwa serikali ni kuweka mikakati madhubuti ambayo itawasaidia kuwakomboa wakulima wa zao la muhogo hivyo ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa ni mkombozi mkubwa na chachu ya kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Pia Ndikilo, amewataka maofisa ugani waliopo Mkoani humo kujenga tabia ya kuwatembelea wakulima wa zao la muhogo ili waweze kutoa elimu ya namna ya uzalishaji wa zao hilo.
Alisema ,zao la Muhogo ni moja ya zao muhimu na kwamba likitumika vizuri linaweza kuwaongezea wakulima kipato na hata kuongeza kipato cha Mkoa na hata kujenga uchumi wa Taifa.
Ndikilo ,alisema kuwa wakulima wengi
wanalima zao hilo huku wakiwa hawana utaalamu
wala elimu ya kutosha juu ya zao hilo na kwamba ni wakati wa maafisa
ugani kuona namna ya kuwatembelea wakulima kwa kuwapa elimu ya zao hilo.
Aliongeza kuwa,mkoa wa Pwani unajumla
ya hekta 3,353,900 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 1,933,224 sawa na
asilimia 57.66 ya eneo lote.
Alisema, pamoja na kuwepo kwa ukubwa wa eneo hilo lakini bado Muhogo hulimwa kwa kiasi kidogo ikiwa ni wastani wa hekta 60,703 na kuzalisha tani 500,000 hadi 650,000 kwa mwaka huku akisema eneo hilo ni asilimia tatu.
" Kwa upande wa tija nayo ipo chini kwa miaka mitano iliyopita
uzalishaji kwa eneo ni wastani wa tani 6.5 hadi 7.6 kwa hekta ingawa yapo maeneo machache hasa Kibiti na
Rufiji ambako tija ni kati ya tani 9 hadi 18 kwa hekta wakati tija
inayopendekezwa kitaalamu kuwa ni tani 20 kwa hekta" alisema Ndikilo.
Kuhsu usindikaji mkuu huyo wa mkoa
alisema mkoa bado haufanyi vizuri pamoja
na kuwepo kwa juhudi za kuanzisha vikundi na Viwanda vya usindikaji kwani
vikundi 32 vilivyopo katika Mkoa huo havisindiki mihogo kwa madai ya kukosa
soko la uhakika.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wadau wa Zao
la Muhogo (TACAPPA) Mwantumu Mahiza, alisema endapo wakulima watahamasishwa
kuhusiana na zao hilo litawasaidia kujikwamua kutoka kwenye umasikini.
Mahiza, alisema maaofisa ugani
wanatakiwa kusaidia kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kulima zao hilo
kitaalamu na kupata mbegu bora na kwamba bila hivyo hakuna mafanikio
yatakayopatika.
Alisema,chama hicho kimejipanga
kupambana na vikwazo vya soko la zao hilo ambapo vikitolewa wakulima
watachangia kuinua uchumi wa taifa na kuondoa umasikini wa kaya.
Mahiza,alisema kuwa kwasasa Taccapa
kipo katika mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha Muhogo ambacho kitahudumia
Mikoa ya Kanda ya Mashariki na Kati na kufanya Muhogo kupata soko kubwa zaidi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa
wa Pwani Dkt.Dolphine Magere,alisema kuwa kikao hicho kinalenga kutoa dira ya
kuhakikisha zao Muhogo linapata hadhi kama mazao mengine.
Magere,alisema baada ya kikao hicho
timu mbalimbali kupitia Halmashauri zitaundwa kwa kuwashirikisha maafisa ugani
ili kusudi wawe karibu na wakulima wa zao hilo.
Mmoja wa wakulima aliyeshiriki kikao hicho Gosbert Joshua aliomba kuwepo na kituo cha kuzalisha mbegu za Muhogo kuondoa usumbufu wa kuzifuata mbali na wanapoishi.
Mwisho.
0 Comments