Na Shushu Joel, Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewakaribisha na kuwahakikishia wawekezaji wa ndani na nje mazingira mazuri ya uwekezaji katika Mkoa huo wa Pwani.
| Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kuwekeza Pwani(NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa ofisini kwake akizungumza na Mwandishi wa habari wa Blog na online tv ya HABARI MPYA.
Kunenge alisema kuwa Mkoa wa Pwani bado una fursa nyingi za uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania wenye dhamira ha kuwekeza Mkoani humo.
"Pwanj ni Mkoa wa pekee uliobarikiwa kuwa na maeneo mengi na yenye tija kwa uwekezaji hii inatokana na uwepo wa mali Ghafi za kutosha na mazingira mazuri ya uwekezaji" Alisema Mkuu wa Mkoa Kunenge
Aidha aliongeza kuwa mpaka sasa katika Mkoa wa Pwani kuna viwanda visivyo pungua 1000 lakini bado tuna maeneo mengi na ya kutosha kwa wawekezaji hivyo niwaombe waweze kuja katika Mkoa huu .
Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mkoa wa Pwani Bi' Halma Mdoe mara baada ya mahojiano hayo alisema kuwa uwepo wa Mkuu huyo wa Mkoa hapa Pwanj kumefungua ajira kwa vijana wetu na bado zitaongezeka kutokana na kuwa Mkuu wa Mkoa bado anasisitiza watu kuwekeza Pwani.
Aidha amemtaka kuendelea na moyo huo katika Mkoa wetu kwani amekuwa akijitolea kwa vitu vingi ili Mkoa wetu usonge mbele katika nyanja za maendeleo.
MWISHO
0 Comments