NA SHUSHU JOEL
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameungana na Watanzania kuipongeza klabu ya Yanga kwa hatua ya nusu fainali waliyofikia katika mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanua jambo Bungeni kuhusu timu za Yanga na Simba
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema hayo Mei 11, 2023 Bungeni jijini Dodoma ikiwa ni utaratibu
aliojiwekea katika mikutano ya Bunge kila siku ya Alhamisi kupata wasaa wa kujibu
maswali ya Wabunge ya papo kwa papo ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali.
“Hakika
Dar Young Afrika inaendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania, na niwapongeze
sana kwa matokeo ya jana, tunawaombea kwa mchezo wa marudiano kule Afrika
Kusini mshinde kwa magoli mengi” amesema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa Watanzania wanahamu ya kuona Tanzania inaingia
kwenye mashindano hayo ya CAF kwenye ngazi ya fainali.
Aidha,
Waziri Mkuu ameipongeza timu ya Simba kwa hatua iliyofika ambapo amesema anaamini
wamejifunza kutoka kwa klabu jirani na hatua waliyofika huku akiamini msimu ujao
vilabu viwili au zaidi vifanye vizuri zaidi.
Katika
msimu wa 2022/2023 timu za Tanzania za Yanga na Simba zimefanya vizuri
kwenye
mashindano ya Afrika kwa timu ya Yanga hadi sasa ipo hatua ya nusu fainali
Kombe
la Shirikisho Barani Africa (CAF) na timu ya Simba ikifikia hatua ya robo
fainali
ya
kombe la Klabu Bingwa Afrika.
0 Comments