HAJAT MARIAM ULEGA ACHANGIA MILIONI 31 UJEZI NYUMBA YA WATUMISHI WA UWT .


Na Shushu Joel, Kibaha 


MJUMBE wa Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa na Mbaraza wa Jumuiya hiyo Hajat Mariam Ulega amechangia jumla ya kiasi cha  shilingi Milioni 31kwa ajili ya Nyumba za watumishi wa Jumuiya hiyo ya UWT katika Mkoa wa Pwani.


Akizungumza na HABARI MPYA MEDIA Hajat Mariam Ulega alisema kuwa kusudi lake kubwa la kuchangia kiasi hicho cha pesa ni kuondoa changamoto ya kukosekana kwa makazi kwa watumishi wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Pwani.


Akitoa ufafanuzi juu ya uchangia huo Hajat Mariam Ulega alisema kuwa Ujenzi wa Nyumba ya katibu wa uwt Mkoa ametoa Milioni 5, Ujenzi wa Nyumba ya Katibu Uwt Bagamoyo Milion 6,Ujenzi wa Nyumba ya Katibu Uwt Mkuranga Milion 5, Ujenzi Nyumba ya katibu Uwt Rufiji Milion 4, Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa Uwt Kibiti Milion 1,Ujenzi  katibu Kisarawe Milioni 2, Mafia Milion 1, Kibaha Vijijini Milion 1 na Ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT wilaya ya Kibaha Mjini Milion 6 Hivyo kupelekea jumla ya milioni 31 za ujenzi wa Nyumba hizo.


Aidha alisema kuwa atahakikisha Nyumba hizo zinakamilika na watumishi hao wanahamia kwenye makazi yao mazuri na wafurahie kufanya kazi katika Mkoa wa Pwani.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini Mama Mgonja amempongeza Hajat Mariam Ulega kwa kuwa nguzo ya jumuiya hiyo huku akisema hakuna kama Mama Ulega.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments