Na Shushu Joel, Rufiji
MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi,Nadra Ghulam amewataka wananchi kutokuwa waoga pindi wanapofanyiwa ukatili wa aina yeyote ile.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani ambapo Jumuiya hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mery Chatanda inafanya ziara ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Bi, Nadra alisema kuwa kumekuwepo kwa matukio ya ukatili kwa watoto na hata watu wazima jambo ambalo si sahihi kabisa na kama wazazi kila mmoja wetu ana haki ya kulikemea jambo hilo.
Pia amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani ndio Chama pekee chenye Sera na dira ya kuliongoza Taifa hili.
"Kila Mtanzania anaona kile ambacho Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anakifanya katika maendeleo hivyo watanzania watampa kura za kishindo Rais Samia ili aendelee kuwaneemesha watanzania"Alisema Mnec Bi, Nadra Ghulam Mnec
Katika ziara hiyo Bi, Nadra Ghulam ametembelea kituo cha Afya cha Ikwiriri na ujenzi wa chuo cha ufundi unaendelea na pia ameshiriki katika ujenzi huo kwa kuonyesha ishara ya kazi na utu.
MWISHO
0 Comments