Na Shushu Joel, Kibiti
MJUMBE wa Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa na Mbaraza wa Jumuiya hiyo Hajat Mariam Ulega ametimiza ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa Wilaya wa jumuiya hiyo.
Akikabidhi fedha hiyo ya ujenzi wa nyumba hiyo katika Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Bi, Nyemo Mwaka alisema kuwa amemwakilisha Mbaraza kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa nyumba hiyo.
Aliongeza kuwa Hajat Mariam Ulega aliahidi kiasi cha shilingi Milioni Moja ili kufanikisha zoezi la ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT katika Wilaya ya Kibiti ili kufanikisha kuondoa changamoto ya makazi kwa watumishi wa Jumuiya hiyo.
Aidha Mwakilishi huyo wa Hajat Mariam Ulega amewataka wajumbe wa kamati ya utekelezaji kuendelea kumuombea Dua Mbaraza ili aendelee kuisaidia jumuiya hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibiti Bi, Tatu Mkumba amempongeza Mbaraza Hajat Mariam Ulega kwa ufanikishaji wa ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya mtumishi kiasi cha shilingi milion moja.
Kwa kweli Hajat Mariam Ulega amekuwa msaada mkubwa kwenye jumuiya ya UWT katika Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla.
MWISHO
0 Comments