UWT KISARAWE WAMPA TANO HAJAT MARIAM ULEGA


Na Shushu Joel, Kisarawe 


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Bi, Asia Madima amempongeza Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania Hajat Mariam Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha watumishi wa jumuiya wanakuwa na nyumba za kuishi.

Hayo amesema alipokuwa akipokea fedha kiasi cha shilingi milion moja kutoka kwa Mbaraza ambazo aliahidi kutoa ili kusaidia ujenzi wa katibu wa UWT wilaya ya Kisarawe.


" Hajat Mariam Ulega amezidi kuwa kiongozi mwenye uchu wa maendeleo hasa ya UWT jambo ambalo limeifanya jumuiya hiyo kuwa na mvuto mkubwa katika Mkoa wa Pwani " Alisema Asia Madima 


Kwa upande wake mwakilishi wa Hajat Mariam Ulega amekabidhi fedha hizo kwa viongozi hao ili ziweze kufanikisha ujenzi huo wa nyumba za mtumishi wa jumuiya hiyo katika Wilaya ya Kisarawe. 


Aidha amewataka kuzitumia pesa hizo kwa lengo lililokusudiwa ili watumishi wetu waondokane na changamoto ya ukosefu wa nyumba.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments