Na Shushu Joel, Musoma
MJUMBE wa Baraza la Wazazi Taifa viti vitatu Bara Ndg Ally Mandai ameipukutisha ngome ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) Wilaya ya Musoma Mkoani Mara kwa kuvuna wanachama wa chama hicho zaidi ya 20.
Ngome hiyo imepukutishwa na Ndugu Mandai kupelekea wananchi hao kuelewa kazi inayoendelea kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan hapa Nchini.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wazazi katika Wilaya hiyo Mandai alisema kuwa hakuna mtu asiyeyaona maendeleo makubwa yanayofanywa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha Mandai amewapongeza wote waliofanya maamuzi sahihi ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani ndio chama pekee hapa Nchini kinachowajali wananchi wake kwa kuwatimizia maendeleo ya jamii.
Pia Mjumbe huyo wa Baraza la Wazazi Taifa viti vitatu Bara Ndg Mandai amewataka viongozi wa CCM na wanachama kuendelea kuwa karibu na wale wote waliorejea katika chama kikubwa ili waelewe dhamira ya Mwenyekiti wetu na Rais Dkt Samia katika kuwaletea maendeleo watanzania.
Naye Amina Chacha amempongeza Ndg Mandai kwa hotuba safi na iliyojaa hekima na busara.
Aidha amemuomba Ndg Mandai kufikisha salamu za dhati kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani anayoyafanya kwa Taifa letu.
MWISHO.
0 Comments