DC SHAKA AWATAKA WAZAZI KUWALINDA WATOTO NA VITENDO VYA UKATILI


Na Mwandishi wetu  Morogoro 

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amewataka Wazazi , walezi, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa maendeleo kukumbuka jukumu  lao la kuwalinda watoto ili kuwajengea ustawi wa kesho kwa kuwaunda kuwa watumishi bora katika Taifa la kesho.


Mhe. Shaka ameyasema hayo Juni 16, 2025 akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa Wilayani Kilosa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kilosa Town ambapo amesema wazazi wanatakiwa kukaa karibu na watoto ili kujua wanayoyapitia na wawe huru kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo viovu.


Sambamba  na hayo amewataka  Maafisa   Maendeleo  na Ustawi wa jamii katika ngazi ya Halmashauri  na Kata waendelee kuimarisha elimu, malezi na makuzi ya watoto kwa wazazi na walezi ili waelewe wajibu wao wa kuwalea watoto kwa kuzingatia misingi  ya haki na usawa wa kijinsia.


Aidha Shaka ameongeza kwa kusema kuna ripoti mbalimbali zimeeleza kuwa  bado  watoto  wanakabiliwa na changamoto za vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali  ikiwemo ubakaji, ulawiti, utumikishwaji  katika ajira hatarishi, utekaji, vipigo, kuchomwa moto, mimba za utotoni na ukatili wa mitandaoni ambapo  katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa serikali kwa kushirikiana na wadau imefanya  jitihada za kuratibu na kusimamia program ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto kwa mwaka 2020/ 2025.


Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii  Mkoa wa Morogoro  Gibson  Mwakoba amesema maadhimisho hayo yametokana  na tukio la Mauaji  ya watoto elfu mbili ambalo   lilitokea  Juni  16, 1976 katika  Kitongoji cha Soweto  Nchini  Afrika Kusini  ambapo mauaji hayo yalitokea baada ya watoto hao kuamua kuandamana  kudai haki  yao ya kutobaguliwa sawasawa na wengine hivyo  Jamii  na wazazi  wote wanapaswa kuhakikisha  kuwalinda Watoto  dhidi ya vitendo vya ukatili.


Maadhimisho  hayo  yamehudhuriwa  na Viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata Wadau mbalimbali wa maendeleo, watoto na wananchi kwa ujumla yakiambatana na kauli mbiu isemayo “HAKI ZA MTOTO ,

Post a Comment

0 Comments