Na Shushu Joel, Bunda.
KATIBU wa Siasa na Itikadi wa kata ya Balili Wilaya ya Bunda Mkoani Mara Ndugu Edward Nyamanyi amewataka wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania uongozi mbalimbali mara kipyenga kitakapopulizwa .
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Blog ya HABARI MPYA alisema kuwa ni vyema kwa wale wenye sifa kuchukua fomu na kuweza kuomba nafasi hizo.
Aidha amesema kuwa ni vyema wananchi na wanachama kuendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwani ndio chama pekee chenye maono na dira ya maendeleo kwa watanzania.
"Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi mwenye maono makubwa na Taifa letu hivyo ni vyema kumpatia viongozi ambao wanatokana na ccm ili waweze kuongea Lugha moja kwenye vikao" Alisema Mwenezi Nyamanyi.
MWISHO
0 Comments