MWENGE WA UHURU WAKOSHWA NA MIRADI YA ZAIDI YA BILIONI 9 MKURANGA


Na Shushu Joel, Mkuranga 


KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi ameisifu Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa kuwa na miradi ambayo ni kipaumbele cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 



Akizungumza na Wananchi waliojitokeza kushuhudia mbio za Mwenge wa Uhuru Ussi alisema kuwa Wilaya ya Mkuranga imegawa majiko ya Gesi ili kusaidia wananchi kuweza kutumia Nishati bora kama vile ambavyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza katika matumizi bora ya utumiaji wa Nishati hiyo.


Aidha kiongozi huyo wa mbio hizo za Mwenge amewapongeza viongozi  wa Mkuranga kwa umoja na ushirikiano katika ujenzi wa Mkuranga pasipo changamoto yeyote ile kwa jamii.


Pia amewasifu wawekezaji ambao chanzo chao kikubwa ni Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ya uwekezaji jambo ambalo limekuwa na manufaa makubwa kwa Wilaya ya Mkuranga kuzidi kuwa na Viwanda lukuki.


Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Khadija Nasiri amezidi kuwa kiongozi muunganishi baina ya wananchi na seeikali kitu ambacho kimedi kumfanya kuwa kipenzi cha wananchi wa Mkuranga. 


Aidha amewapongeza wananchi wa Mkuranga kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia Mwenge wa Uhuru unavyowaka na kumelemeta .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments