Na Shushu Joel, Dar
CEO wa kampuni ya Tremendous Catalogue ya Jijijini Dar es Salaam Bi, Batuli Omary amesema kuwa heshima kubwa inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni kubwa sana na isiyo ya kifani.
Akizungunza na HABARI MPYA BLOG alisema kuwa Rais Dkt Samia anatuonyesha upendo wa pekee watanzania katika kutuletea maendeleo mbalimbali ndio maana vijana tulio wengi tumekubaliana kumpa mitano tena.
Aidha Batuli alisema kuwa kila kona ya nchi yetu Rais Dkt Samia amefanya maendeleo ya kutosha na yenye uhakika wa huduma kwa jamii.
" Niwaombe Vijana , Wanawake na Wanaume msidanganyike na watu wasio litakia mema Taifa letu sote kwa pamoja tukampe heshima ya pekee Rais Dkt Samia katika uchaguzi ujao" Alisema Bi, Batuli
MWISHO
0 Comments