"RAIS DKT SAMIA AUNGWE MKONO KWA JUHUDI ZA KULETA MAENDELEO " MNEC NADRA GHULAM

 

Na Shushu Joel, Zanzibar 


MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM)   Taifa anayetokana na Umoja na Wanawake Tanzania Bi, Nadra Ghulam amewataka watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo anayoyafanya.

Akizungumza na Wananchi Mnec Nadra alisema kuwa kila mtanzania anayo haki ya kumsemea Rais Samia kwa kile anachokifanya kwa watanzania.


Aidha alisema kuwa Rais Dkt Samia amekuwa Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amefanya mambo makubwa kuliko watangulizi wake hii ni kutokana na kuwa na uchungu wa maendeleo kwa watanzania.


Hivyo Bi, Nadra Ghulam Mnec ameeleza kuwa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia imekuwa na mafanikio ya kujivunia kila mmoja wetu.


Naye Ally Mwalami amempongeza Mnec Nadra kwa kuwa kiongozi mwenye maoni na upendo kwa wale anaowaongoza.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments