MHE MGALU AKOSHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

Na Shushu Joel, Rufiji. 

MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Mhe Subira Mgalu  ameridhidhwa na ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kujenga na ile iliyokamilika katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani. 


Haya ameyasema alipotembelea katika kituo cha Afya cha Ikwiriri na katika ujenzi unaoendela wa shule ya ufundi .


Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mhe Mgalu alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa ambayo wananchi wamezidi kujivunia uwepo wa miradi hiyo.


"Kwa jinsi ambavyo Rais Samia anavyopeleka maendelea sehemu mbalimbali za nchi hii ni wazi kabisa uchaguzi ujao Dkt Samia anakwenda kuvunja rekodi ya kupata kura nyingi na za kutosha kutoka kwa watanzania" Alisema CPA Mgalu.


Aidha Mhe Mgalu amewaomba wananchi wa wilaya ya Rufiji kuendela kuitunza miradi hiyo ili iendelee kutumiwa na vizazi vijavyo .


Kwa Upande wake Eng Bakari Ally ambaye ni mjenzi wa mradi huo wa shule ya ufundi amempongeza Mhe Mgalu kwa ushauri wake juu ya ujenzi wa shule hiyo huku akisisitiza kukamilika kwa haraka ili watoto waanze kupata mafunzo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments