Na Shushu Joel, Mkuranga.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amezidi kuwa ni kielelezo kwa Wanawake Nchini na Dunia kwa ujumla kutoka na utendaji wake mkubwa uliotukuka.
Haya yameelezwa na Mtendaji wa kata ya Shungubweni Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Bi, Asha M. Dilunga alipokuwa akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Shungubweni katika mahafali ya kwanza ya shule hiyo ambaye imeongezewa madarasa mapya sita na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Hakuna mtu yeyote nchini wala nje ya mipaka ya Tanzania ambaye hakioni kile kinachofanywa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan hivyo wazi kabisa Wanawake tunaweza kuleta maendeleo kwa kiwango cha hali ya juu sana" Alisema Mtendaji huyo wa Shungubweni.
Aidha amewataka watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais huyo ili aweze kuyafanilisha yale matarqjio yake na kukata kiu ya watanzania kabisa katika maendeleo.
Pia amewataka watanzania kuendelea kumwamini na kumpigia kura za kishindo ili aendelea kututumikia kwa kipindi kingine.
Naye Fatma Ally Mkazi wa Shungubweni amempongeza Mtendaji huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo na kuwaweka wana jamii katika umoja.
MWISHO

0 Comments