MNEC MLAO ATOA SOMO KWA WANA SIASA

Na Shushu Joel,Mkuranga 


MNEC kundi la Vijana Ramadhani Mlao amewataka wana siasa kuacha tabia za chuki kwa wenzao pindi wanapopata nafasi za uwakilishi kwa wananchi .

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na umati wa wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani. 


Aliongeza kuwa watu wamekuwa na wivu sana pale mwenzao anapopata nafasi jambo ambalo limekuwa likikwamisha maendeleo  hivyo ni vyema kutiana moyo pale mwenzako  anapofanya vizuri katika kuhudumia jamii.


"Visokolakwinyo si vizuri kwa maendeleo ya Taifa letu " Alisema Mnec Mlao.


Aidha amewataka wana ccm kuungana kwa pamoja na kumpigia kura za kishindo Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluhu Hassan ili aendeleze maendeleo kwa Watanzania.


Pia Mnec huyo amemuombea kura Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mkuranga na Madiwani wa kata zote za wilaya hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi. 


Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amempongeza Mnec huyo kwa ujumbe mzito wenye mafunzo kwa wana siasa.


Aidha Waziri Uleza amemwakikishia Mnec huyo kuwa kuwa ccm inaenda kupata ushindi wa kishindo na hasa kura za mgombea wa Urais wa ccm Dkt Samia Suluhu Hassan. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments