NAIBU WAZIRI MASANJA APINGA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Na Shushu Joel

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja na Mbunge wa Viti

Maalum Mkoa wa Mwanza amesikitishwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia

ambavyo ni moja ya kisababishi cha watoto kuishi katika mazingira hatarishi.

Akizungumza katika hafla ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira

hatarishi iliyofanyika Kata ya Mabatini Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza,

amelaani vitendo hivyo na kuwataka wananchi wa Mwanza kuunga mkono

juhudi za kupambana na vitendo hivyo.



“Hatuna budi kuhakikisha kwamba tunawaunga mkono wadau wote

wanaoshiriki katika kutokomeza vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa hali na

mali ili watoto wetu wawe na afya nzuri ya akili na wapate malezi bora” Mhe.

Masanja amesisitiza.


Aidha, ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa

akishiriki katika kuwalinda na kuwatunza watoto hasa wanaoishi kwenye

mazingira magumu. 

Amewapongeza wadau wote waliochukua jukumu la kulea watoto wanaoishi

katika mazingira magumu na hatarishi na kuwataka kutoacha kufanya hivyo kwa

manufaa ya Taifa.


Hafla hiyo ilisaidia kupatikana kwa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni

1,890,000 zilizochangwa na wadau ambapo Mhe. Masanja alitoa fedha taslim

kiasi cha shilingi milioni 1.5 kuchangia gharama za shule kwa watoto hao.

Michango mingine iliyotolewa na wadau ni sabuni, sukari, unga wa lishe,

madftari na kalamu.

Post a Comment

0 Comments