"NITAENDELEA KUWA CCM HATA KAMA NIMESHINDWA KUWA M/KITI " LATIFA


Na Shushu Joel, Bagamoyo 


ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Umwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Bi,  Latifa Kizota amesema kuwa ataendelea kuwa mwana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hata kama kura zake hazikutosha kuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Bagamoyo. 



Akizungumza na HABARI MPYA MEDIA Latifa alisema kuwa sio kila unapogombea nafasi yeyote ile katika Chama lazima ushinde kwani wanachama ndio wenye maamuzi ya kutaka nani awe kiongozi na kwa kipindi gani .


Aidha aliongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Mwenyekiti Mlawa kama vile muongozo wa chama unavyosema kuhusu.


Katika Uchaguzi huo Bi, Latifa alishika nafasi ya tatu huku akiwa ni Mwanamke pekee aliyefanikiwa kuomba nafasi hiyo.


" Wanawake tusiogope kuomba nafasi za uongozi kwani uwezo tunao ndio maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan amezidi kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa ufanisi mkubwa wa maendeleo kwa Watanzania" Alisema Bi, Latifa.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Abubakari Mlawa amempongeza Latifa kwa kuwa Mwanamke mwenye kuthubuti katika chama.


Aidha amewahakikishia wana ccm kuwa atazidi kuwa kiongozi mwenye mwenye maadili mema na mwenye maono makubwa kwa kukitumikia chama cha mapinduzi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments